Bomu jengine lauwa watu Jos, Nigeria

Mshambuliaji aliyejitolea mhanga aliripua bomu kwenye gari nje ya kanisa katika mji wa Jos, katikati mwa Nigeria.

Watu kama 10 wameuwawa.

Hilo ni shambulio la pili kutokea Jos katika majuma mawili.

Wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram walisema walifanya shambulio la mwezi uliopita, ambapo watu watatu waliuwawa na kuwajeruhi karibu 40 wengine.