Ajali ya basi yaua watoto 22

ajali ya basi uswizi
Image caption ajali ya basi uswizi

Watu 28 , wakiwemo watoto 22 wameuawa katika ajali ya basi kusini mwa Uswizi.

Ajali hio ilitokea jumanne usiku basi hilo lilipokua likirejesha wanafunzi nyumbani Ubelgiji baada ya mapumziko na michezo ya kuteleza kwenye theluji katika milima ya Alps.

Polisi ya Uswizi inasema wana amini basi hilo liligonga ukingo wa barabara ndani ya shimo la chini kwa chini kabla ya kupoteza njia na kugonga ukuta.

Hali ya kutatansha bado imetanda kilichosababisha ajali hio, ambayo ni mbaya kuhusisha basi la abiria nchini Uswizi katika kipindi cha miaka 30.

Ajali hio ilitokea ndani ya barabara ya ndani ya shimo la nchini kwa chini karibu na mji wa Sion - Hakuna gari jingine lililohusika.

Yumkini basi hilo lilipoteza muelekeo na kugonga ukingo wa barabara kisha likagonga ukuta likiwa linakwenda kwa kasi kubwa.

Watu 28 kati ya abiria 52 waliokua wakisafiria gari hilo walipoteza maisha yao.

Abiria wengine 24 walionusurika walijeruhiwa, na sasa wamehamishiwa kwenye hospitali mbalimbali za Uswizi.