Demjanjuk amefariki

Mhalifu wa vita wa Ki-Nazi, John Demjanjuk, amefariki Ujerumani akiwa na umri wa miaka 91.

Haki miliki ya picha b

Alihukumiwa mwaka jana kwa kushiriki kwenye mauaji ya watu 28,000 katika kambi ya Wa-Nazi wakati wa vita vya pili vya dunia, huko Sobobor, Poland.

Alihukumiwa kifungo cha miaka mitano, lakini alifunguliwa kwa sababu ya umri wake.

Amefariki kwenye nyumba ya wazee.

Demjanjuk alizaliwa Ukraine, na baada ya vita alihamia Marekani.

Baada ya kunyang'anywa uraia wa Marekani alipelekwa Ujerumani miaka mitatu iliyopita.