Ndege zashambulia kusini mwa Somalia

Inarifiwa kuwa ndege za kijeshi zimeshambulia kambi ya kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab, kusini mwa Somalia.

Haki miliki ya picha internet

Wenyeji wa huko wameiambia BBC kwamba mtu mmoja alikufa, na wengine kadha kujeruhiwa, kwenye kijiji cha Daytubaako, kiomita 15 kutoka Jilib.

Wanajeshi wa Kenya na Ethiopia wako kusini mwa Somalia.