Mabomu mengi yagunduliwa Afghanistan

Wakuu wa usalama katika serikali ya Afghanistan wanasema wamekamata shehena kubwa ya mabomu katika sehemu mbalimbali za nchi.

Haki miliki ya picha Reuters

Tani kama mbili na nusu za mabomu zilikutikana karibu na nyumba ya gavana huko Mazar-e-Sharif, kaskazini mwa nchi.

Watu 6 wamekamatwa.

Wakuu wanasema washukiwa wakipanga shambulio siku ya mwaka mpya wa Nairuz, Jumaane, na wanasema kugundua njama hiyo, kumeinusuru nchi na umwagaji damu mkubwa.

Na katika mji wa Jalalabad, kaskazini mwa Afghanistan, zaidi ya tani 9 za mabomu zilipatikana, zimefichwa kwenye shehena ya ndizi kutoka Pakistan.