Muamba anatambua familia

Haki miliki ya picha getty
Image caption Fabrice Muamba

Fabrice Muamba sasa anaweza kutambua familia na jamaa zake na hata kuweza kujibu maswali. Hii ni kwa mujibu wa wakuu wa kilabu yake Bolton Wonderers pamoja na madaktari.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, pia anaweza kupumua bila usadizi wa mashine , lakini hali yake ingali mbaya kiasi cha kusalia katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Mwamba alianguka uwanjani na kuzimia mnamo Jumamosi wakati wa mechi kati ya klabu hiyo na Spurs.

Moyo wake Ulisimama kwa masaa mawili lakini tangu hapo ameanza kuonyesha dalili za kuimarika kiafya.

Madaktari wamesisitiza kuwa hali ya Muamba sio mahututi lakini ni mbaya.

Muamba anaweza kuinua mikono yake na miguu, ingawa madaktari hawawezi kuelezea kuhusu hali yake ya baadaye kwa sasa.

Mchezaji huyo aliwahi kuchezea timu ya taifa ya Uingereza ya vijana walio chini ya umri wa miaka 21.