Mohamed Mera alitoroka jela Afghanistan

Habari kutoka Ufaransa zasema kua mshukiwa wa mauwaji ya watu saba nchini Ufaransa, Muhammed Merah ameiambia polisi kua alitenda matendo hayo kwa kulipiza kisasi mauwaji ya watoto wa Kipalestina na kuiadhibu Ufaransa kwa kushiriki vita nchini Afghanistan.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi Ufaransa wazingira mhalifu

Waziri mkuu wa Palestina, Salam Fayyad, amesema kua wahalifu wakome kutumia jina la Palestina kuhalalisha vitendo vyao.

Wakati huo huo nchini Afghanistan imearifiwa kua mtu mwenye jina la Mohammed Merah alikua miongoni mwa wafungwa waliotoroka baada ya shambulio la Taliban kwenye Jela mnamo mwaka 2008.

Wakuu wa usalama nchini Afghanistan wameiambia BBC kua ni mtu huyo huyo anayetuhumiwa kwa mauwaji ya watu saba nchini Ufaransa.

Uwezekano wa kutoroka jela huko Kandahar mnamo mwaka 2008 kulifuatia mpango mzuri na shambulio lililofanikiwa la Taliban.

Kwanza, watu waliojitoa mhanga maisha yao waliendesha pikipiki hadi milango na kuibomoa.

Hawa walifuatiwa na wapiganaji kwa makumi waliosafirisha mahabusu kwenye pikipiki zao na kuondoka nao.

Mkurugenzi mtendaji wa Jela hio, Gulam Farooq ameiambia BBC kua miongoni mwa waliotoroka ni Mohammed Merah, ambaye amethiubitisha ndiye aliyeua watu saba nchini Ufaransa.

Alikamatwa akiwa nchini Afghanistan ya kusini akiwa na vifaa vya kuunda bomu na kuhukumiwa miaka mitatu jela.

Maofisa wa ujasusi wamewasiliana na idara ya usalama ya Afghanistan ikitaka taarifa zaidi kumhusu mtuhumiwa.