Jeshi laasi nchini Mali

Image caption Waasi wa Tuareg

Makabiliano makali yametokea katikati ya mji mkuu wa Mali, Bamako, baada ya magari ya kijeshi yenye silaha kuzingira ikulu ya rais.

Mwandishi wa BBC mjini Bamako, Alou Diawara, ameelezea kuwa kituo cha televisheni cha serikali kimetekwa na wanajeshi waasi na kuzima matangazo.

Hatia hii ya jeshi imetokea wakati kukiwa na mgogoro katika jeshi kuhusu namna ya kukabiliana na waasi wa Tuaraeg walioko kaskazini mwa nchi wanaosemekana kukaribia mji mkuu.

Mapema waliteta vikali kuhusu uchache wa silaha katika jitihada zao dhidi ya waasi wa Tuareg na kwamba wanapinga majadiliano yoyote na waasi hao.

Duru zinaarifu kuwa wanajesi hao wamevamia makao makuu ya shirika la utangazaji la serikali.

Mapema leo wanajeshi walifyatua risasi hewani, wakati waziri wa ulinzi wa nchi hiyo akianza kutembelea kambi za jeshi kaskazini mwa mji mkuu Bamako.

Aidha mapema wiki hii, shirika la nchi za magharibi, Ecowas, liliwataka wanachama wake kusaidia jeshi la mali kwa Silaha na uwezo wa mipangilio juu ya namna ya kuendesha harakati zao dhidi ya waasi wa Tuareg.