Ngozi kugombea urais wa benki ya dunia

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Bi Ngozi Okonjo Iweala

Mawaziri wa fedha wa nchi tatu barani Afrika, wamekubaliana kumteua waziri wa fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo Iweala kuchukua nafasi ya rais wa Benki ya Dunia.

Nchi hizo ni Nigeria, Angola na Afrika Kusini.

Ngozi Okonjo-Iweala, ambaye ni waziri wa fedha nchini humo, amesema anataka kuchukua nafasi ya Robert Zoellick aliye rais wa sasa wa benki hiyo.

Uteuzi unakamilika leo. Mwandishi wa BBC wa maswala ya biashara, anasema kuwa Bi Ngozi Okonjo-Iweala ana sifa nzuri na inayoweza kumfanya kupata nafasi hiyo.

Hata hivyo wadhifa wa mkuu wa benki umekuwa ukimwendea Mmarekani tangu kuudwa kwake mwaka 1944.