Bunge la Misri lateua tume ya katiba

Bunge la Misri linateua tume ya wajumbe 100 kutayarisha katiba mpya.

Haki miliki ya picha AP

Baada ya uchaguzi wa kwanza tangu Hosni Mubarak kuondolewa, wajumbe wengi katika bunge la sasa ni wa vyama vya Waislamu, na vyama vidogo vya siasa vimesema vina wasiwasi kuwa vitagubikwa kwenye majadiliano hayo.

Katiba mpya itaeleza mezani ya madaraka baina ya bunge na rais.

Chama kimoja kikuu cha Waislamu, Muslim Brotherhood, kinasema kuwa kina hamu kuona kuwa maoni yote ya siasa na itikadi yanawakilishwa.