Papa azuru Mexico

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict, anatarajiwa kuzungumza na Rais Felipe Calderon wa Mexico baadaye leo, katika jimbo la Guanajuato, siku ya kwanza ya ziara yake rasmi nchini Mexico, nchi yenye wakatoliki wengi kabisa duniani.

Haki miliki ya picha Reuters

Papa amesema yeye ni mgeni wa kuleta matumaini.

Amesema anataka kuwasaidia Wamexico kubadilisha maisha yao, na amelaani ghasia zinazohusika na madawa ya kulevya, ambazo zimeuwa maelfu ya wananchi katika miaka ya karibuni.