Malema asema atakwenda mahakamani

Julius Malema, kiongozi wa tawi la vijana la chama tawala cha Afrika Kusini, ANC, amesema ikiwa atashindwa katika rufaa yake kwamba asifukuzwe kwenye chama, atafikisha kesi yake mahakamani.

Haki miliki ya picha AFP

Bwana Malema hapo awali alikataa kuwa atachukua hatua ya kisheria.

Alifukuzwa katika chama cha ANC, mwezi uliopita, kwa sababu alikashifu chama kutokana na matamshi yake kadha ya kibaguzi dhidi ya wazungu, na malalamiko juu ya Rais Jacob Zuma.