Papa aongoza ibada kubwa Mexico

Malaki ya wananchi wa Mexico walikusanyika katika mji wa Silao, kuhudhuria ibada iliyoongozwa na Papa Benedict, ambaye anazuru nchi hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters

Mwandishi wa BBC mjini Silao anasema wakuu wa kanisa la Katoliki wanatumai ibada hiyo itasaidia kuthibitisha tena imani nchini Mexico, ambako makanisa ya wahubiri yamekuwa yakivutia waumini kati ya Wakatoliki.

Jumuia ya Wakatoliki Mexico ni ya pili kwa ukubwa duniani, baada ya Brazil.