Dewani hatarejeshwa SA punde

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Dewani na familia ya mkewe Anni

Ombi la kurudishwa Afrika Kusini kwa mshukiwa wa mauaji katika kesi inayoendelea nchini Uingereza, limesitishwa kwa muda.

Majaji wanaosikiliza kesi hiyo wamesema afya ya mshukiwa Shrien Dewani sio nzuri kwa sasa, na hivyo kubatili uamuzi wa mahakama.

Dewani anadaiwa kuhusika na mauaji ya mke wake wakati walipokuwa wanaishi naye nchini Afrika Kusini. .

Shrien Dewani, mmiliki wa makao ya huduma kwa watu eneo la Bristol,Uingereza, alikata rufaa katika mahakama kuu dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kurejeshwa kwake nyumbani Afrika Kusini ili kuhukumiwa huko.

Anakana kuhusika na mauaji ya mkewe ,Anni, aliyeuawa kwa kupigwa risasi mjini Cape Town, mwezi Novemba, mwaka 2010.

Umuazi wa kurejeshwa kwa Dewani awali uliungwa mkono na waziri wa mambo ya ndani nchini Uingereza ,Teresa May.

Majaji wawili wa mahakama kuu, waliamua kuwa itakuwa kinyume ya haki za mshukiwa na udahlimu kuamuru arejeshwe nyumbani.

Lakini mahakama ikasisitiza kuwa ni sharti Dewani akahukumiwe nchini Afrika Kusini ili haki kutendeka kwenye kesi hiyo , na kwamba hilo lifanyike pindi atakapopata nafuu.