Annan afaa kuweka ratiba Syria

Marekani na mataifa ya Ghuba ya Arabuni yametoa wito kwa mjumbe wa kimataifa, Kofi Annan, aweke ratiba kwa serikali ya Syria kukubali mpango wake wa amani.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano baina ya Marekani na nchi za Ghuba, uliofanywa Saudi Arabia, ilisema juhudi za Bwana Annan ni muhimu - na ratiba ya hatua zitazofwata inafaa kuwekwa, iwapo serikali ya Syria itaendelea kuuwa waandamanaji.

Upinzani unasema mauaji yameendelea.

Hapo awali, msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Syria alieleza kuwa serikali imeshinda jaribio la kuipindua serikali.

Mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu Syria utafanywa Uturuki Jumapili.