Cuba itapumzika Pasaka

Serikali ya Cuba imetangaza kuwa Ijumaa ya Pasaka itakuwa siku ya mapumziko, baada ya kuombwa na Papa Benedict.

Haki miliki ya picha Reuters

Siku hiyo ni muhimu kwa Wakristo wakati wa Pasaka, na Papa alitoa ombi hilo wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini Cuba.

Tangazo lilotolewa na Cuba lilisema kuwa siku hiyo kwanza itakuwa ya mapumziko mwaka huu tu, lakini uamuzi utachukuliwa baadae kama ada hiyo itaendelezwa au la.