Marafiki wa Syria wakutana

Waakilishi wa nchi zaidi ya 70 zinazounga mkono mabadiliko ya kisiasa nchini Syria, wamemskiliza Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, akiishutumu jumuia ya kimataifa kuwa imewatelekeza wananchi wa Syria.

Haki miliki ya picha AFP

Akihutubia mkutano huo mjini Istanbul, alihimiza kuwa madai halali ya Syria yaitikwe haraka.

Hapo awali kiongozi wa upinzani wa Syria, wa Halmashauri ya Taifa ya Syria, SNC, Burhan Ghalioun, alitoa wito kwa jamii ya kimataifa, kuitambua SNC pekee, kuwa mwakilishi halali wa wananchi wa Syria.

Lakini waandishi wa habari wanasema kuna wasiwasi kuhusu mgawanyiko ndani ya SNC.