Saif Al Islam ashambuliwa gerezani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Saif Al Islam

Mawakili wa Saif Al Islam katika mahakama ya kimataifa ya jinai wamedai mteja wao anateswa kizuizini alikofungwa nchini Libya.

Mawakili hao wamesema Saif ametengwa kabisa ambapo pia wapiganaji wanaomzuilia wamekuwa wakimpiga.Viongozi wa mashtaka nchini Libya waliwaarifu mawakili hao kwamba Saif alikabiliwa na makosa madogo ya kukosa leseni ya kufuga ngamia na samaki.

Utawala wa mpito nchini Libya unasisitiza kwamba Saif Al Islam anastahili kufungulia kesi nchini humo japo mahakama ya Hague inashinikiza utawala huo kumkabidhi Saif kwake.

Saif Al Islam ni mwanawe kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi ambaye aliuawa katika mapinduzi nchini mwaka. Ameshtakiwa katika mahakama ya ICC kwa makosa ya kibinadamu kwa kuamrisha mauaji ya raia wakati wa maandamano dhidi ya utawala wa marehemu babake.