Bomu laua watu 12 Baidoa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bomu laua kumi na mmoja mjini Baidoa nchini Somalia

Takriban watu 11 wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya kwa bomu mjini Baidoa katikati mwa Somalia.

Gavana wa jimbo la Bay, Abdifitah Mohamed Gesey, aliiambia BBC majeruhi wengi walikuwa wanawake na watoto.

Bw Gesey alisema bomu liliwekwa katika kikapu kidogo na kufichwa katika eneo la soko lenye shughuli nyingi katikati ya mji.

Ni shambulio baya kutokea mjini Baidoa tangu vikosi vya Ethiopia idhibiti eneo hilo kutoka kwa al-Shabab, mwezi Februari.

Walioshudia walisema bomu lilipuka muda mfupi baada ya vikosi vya serikali ya Somalia kuwasili sokoni hapo.

"Hili lilikuwa ni janga," Adan Hassan, shahidi aliliambia shirika la habari la AFP.

"Niliona miili takriban tisa ya raia wengi wao wakiwa ni wanawake. Mlipuko umetokea wakati watu wananunua mahitaji yao."

Msemaji wa kundi la al-Shabab alisema wanahusika na mlipuko huo.

"Tuliwalenga Waethiopia na vikosi vya Somalia. Wamekufa watatu, " Sheikh Abdiasis Abu Musab aliliambia shirika la habari la Reuters.

Walinda amani

Ni bomu la pili katika kipindi cha chini ya wiki moja.

Jumatano, watu wanane waliuawa katika bomu la kujitoa muhanga katika chumba cha upasuaji cha Taifa Mogadishu.

Wiki iliyopita vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Ulaya kwa mara ya kwanza vilisambazwa mjini maeneo ambayo ni muhimu kimkakati.

Mji wa Baidoa uko kilometa 250km (155 maili) kaskazini magharibi mwa Mogadishu, umekuwa mmoja wa miji muhimu kwa ngome za al-Shabab.

Mji huo umekuwa tangu udhibitiwe miaka mitatu iliyopita chini ya serikali ya mpito ya Somalia.

Al-Shabab ilisema imeondoa vikosi vyakekama ‘mbinu ya kurudi nyuma’ na kutishia kuanza vita vya msituni/mafichoni kujibu mashambulizi.