Baraza la Katiba lasimamishwa Misri

Image caption Baraza la katiba Misri lasimamishwa kupisha rasimu ya katiba mpya

Mahakama nchini Misri imesimamisha Baraza la wajumbe mia moja walioteuliwa mwezi uliopita ili kuandika rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.

Wanasheria waliofungua kesi kadhaa wametaka Mahakama ya Utawala mjini Cairo kuzuia uamuzi wa kuanzisha jopo hilo kwani halikuwa na uwakilishi wa jamii nzima ya Wamisri

Wamesema vijana na makundi mengine madogo hayakuwakilishwa vilivyo.

Makundi ya Waislamu kutoka chama cha Muslim Brotherhood's Freedom and Justice na chama cha Salafist Nour, vinavyotawala bunge yana uwakilishi mkubwa.

Waliberali na watu wasio na mafungamano na dini wana wasiwasi kuwa baadhiyaowanaweza kurekebisha katiba ili ifuate sheria kali za Kiislam sharia.

Muswada huo pia utaeleza iwapo haki za kidini za Wamisri na makundi mengine madogo na ulinganifu wa madaraka kati ya Rais -ambayo awali yalikuwa ndio ya mwisho-na bunge.

Baada ya jopohilokuandaa muswada litatoa rasimu ya mapendekezo. Inategemewa kuwa hiyo itafanyika kabla ya uchaguzi wa Rais Mei.