Kabila sasa ataka Ntaganda akamatwe

Image caption Jenerali Ntaganda anatafutwa na ICC, Rais Kabila atoa wito akamatwe

Rais Joseph Kabila amesema kiongozi wa zamani wa waasi Bosco Ntaganda, anayetafutwa na Mahakama ya Uhalifu ta ICC ni lazima akamatwe.

Lakini Jenerali Ntaganda lazima yuko DRC Rais Kabila anasema.

Bw Kabila awali alikataa wito wa kumkamata mtu huyo aliyejulikana kama"The Terminator".

Mahakama ya ICC kwa miaka mitano sasa inamtafuta kwa kusajili watoto kuwa askari wakati wa miaka mitano ya vita vikali DRC.

'Hukumu ya Goma'

Rais Kabila alifanya mikutano ya dharura na maafisa wa juu wa jeshi mashariki mwa nchi kufuatia mamia ya askari kukimbia jeshi la Kongo.

Askari wanaomtii Jenerali Gen Ntaganda, walijumuishwa katika jeshi la nchi mwaka 2009.

Hata hivyo ndani na kuzunguka Goma ambako majeshi yako wanawalalamikia kuendelea kwa vurugu ikiwemo uporaji na ubakaji tangu kumalizika kwa vita 2003.

"Nataka kumkamata Bosco Ntaganda kwa sababu umati wote wa watu unataka amani," Shirika la Reuters limemukuu Rais Kabila akisema.

"Amefanya uhalifu Kivu ya Kaskazini na Goma…atahukumiwa," alisema.

Mwezi uliopita mwendesha mashataka mkuu wa ICC alitaka Ntaganda akamatwe mara moja baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani kiongozi mwingine wa waasi, Thomas Lubanga, kwa makosa kama hayo.

ICC inasema Jenerali Ntaganda alitumia askari watoto kupigana Ituri kaskazini mashariki mwaCongokuanzia mwaka 2002-2003.

Anatafutwa kwa mauaji na ubakaji.

Waasi hao wa zamani haijulikani wako wapi.

Anaripotiwa kuondoka Goma akichukua pamoja naye askari wenye silaha. Baadhi ya taarifa zinasema askari walioasi 600 walimbatana naye.

Inaarifiwa kuwa wamechukua magari silaha na risasi na mabomu.

Mchambuzi wa BBC wa masuala ya Afrika Martin Plaut anasema kujitenga huko kunaamnisha wazi kuwakamakutakuwa na majribio ya kumkamata Jenerali Ntaganda kutakuwa na shida baadaye.

Msemaji wa jeshi la DRC anasema hatua yoyote ya ukosefu wa nidhamu itakuwa na adhabu yake.