Mutharika arejeshwa nyumbani

Maiti ya Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi, imepelekwa nyumbani kutoka Afrika Kusini, zaidi ya wiki baada ya kufariki.

Mwili wake utawekwa kwa heshima za taifa katika mji mkuu, Lilongwe, na sehemu nyengine za nchi katika siku 9 zijazo; kabla ya kuzikwa shambani mwake huko Thyolo.

Kifo cha Bwana Mutharika kutokana na ugonjwa wa moyo, kilizusha kivumbi cha kisiasa cha siku mbili, kabla ya mpinzani wake, makamo wa rais, Joyce Banda, kuapishwa kuwa rais mpya.