Misri yajaribu patanisha Sudan

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Misri yuko mjini Khartoum kufanya mazungumzo, baada ya siku kadha za fujo kwenye mpaka baina ya Sudan Kusini na Kaskazini.

Waziri huyo, Muhammad Kamil Amr, alisema Misri iko tayari kuchangia kwa namna yoyote ile, kusaidia kumaliza mapambano hayo.

Piya anapanga kwenda Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Siku ya Jumane Sudan Kusini iliiteka Heglig, eneo la Sudan Kaskazini la mafuta.

Hakuna taarifa zaidi za mapigano tangu mji wa Sudan Kusini wa Bentiu kushambuliwa kwa ndege za Sudan Kaskazini Jumamosi.