Aliyeua watu 77 akanusha mashtaka hayo

Imebadilishwa: 16 Aprili, 2012 - Saa 17:54 GMT

Breivik aliwaua watu 77

Mtu anayetuhumiwa kwa mauaji ya watu 77 nchini Norway amekanusha kutekeleza ugaidi na mauaji ya halaiki wakati wa kuanza kwa kesi yake.

Anders Behring Breivik aliambia mahakama iliyofurika manusura na waandishi wa habari kwamba kitendo chake kilikuwa cha kulinda Norway dhidi ya utamaduni wa jamii mbalimbali na kuwepo imani ya Kiisilamu.

Ameongeza hili lilimfanya kutekeleza mauaji ya watu 77 wengi wakiwa vijana katika shambulio la bomu mjini Oslo sawa na kuwapiga risasi vijana waliokusanyika kwa warsha ya chama cha Labour nje ya mji mkuu.

Wakati akiwasili mahakamani Breivik aliinua mkono wake. Alikaa kimya wakati akisomewa makosa yake ambapo pia majina ya waathirika wa mashambulio hayo yalisomwa. Kesi hii inatarajiwa kuchukua wiki 10 na hukumu itatolewa kabla ya mwezi Julai mwaka huu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.