Chemichemi za maji zimejaa Afrika

Image caption Chemchemi za maji afrika

Wanasayansi kwa mara ya kwanza wametoa ramani inayoonyesha kuwepo kwa maji mengi ambayo yamo chini ya maeneo yaliyoko kusini mwa Jangwa la Sahara na maeneo mengine barani Afrika.

Wanasayansi hao wansema maji hayo yamo kwenye chemichemi zilizojaa maji zaidi ya miaka elfu tano iliyopita.

Ripoti inasema maji haya ni muhimu katika kuimarisha kilimo kote Afrika kwa miongo ijayo, lakini tu ikiwa kutachimbwa visima kwa utaratibu unaofaa.

Watafiti hao aidha wanaonya uchimbaji kiholela wa visima huenda ukazikausha chemichemi hizo. Nyingi ya chemichemi hizo zimo Chad, Libya na Algeria.

Zaidi ya watu milioni 300 Barani Afrika wanaishi bila maji safi.