Afghanistan yaepuka mashambulio

Idara ya ujasusi nchini afghanistan inasema imewakamata wapiganaji watano wa Taliban, ambao wakipanga kufanya shambulio kubwa katika mji mkuu, Kabul, juma lilopita.

Haki miliki ya picha AP

Wakuu wanasema washukiwa hao - watatu kutoka Pakistan, na Waafghani wawili, walikamatwa wakiwa na tani kumi za mabomu kwenye lori.

Watu hao walikamatwa kufuatia misururu ya mashambulio mjini Kabul na mikoa mingine mitatu siku ya Jumapili wiki iliyopita, yaliyosababisha vifo vya kama watu 50.

Afisa mmoja wa serikali amesema washukiwa hao wamekiri kuwa wana uhusiano na idara ya ujasusi nchini Pakistan, ISI.