Wasiwasi wazagaa Bahrain

Magari ya deraya na polisi wameshika zamu kwenye barabara za mji mkuu wa Bahrain, Manama, kwa kutaraji maandamano zaidi dhidi ya serikali yatatokea, kabla ya mashindano ya magari ya kimataifa ya Formula One Grand Prix yatayofanywa Jumapili.

Haki miliki ya picha 1

Huku mazoezi ya resi hizo yanafanywa, wanaharakati wa upinzani walisema mtu mmoja amekutikana amekufa.

Wanasema mwanamume huyo, Salah Abbas, alishiriki kwenye maandamano ya Ijumaa.

Wanasiasa na mashirika yanayotetea haki za kibinaadamu wanataka mashindano hayo yavunjwe.

Upinzani unaoongozwa na Washia umekuwa ukijaribu kumuondoa mfalme ambaye ni Sunni, tangu maandamano kuanza Februari mwaka jana.