Libya haitaki kumkabidhi Saif

Serikali ya Libya, imeyaambia Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwamba ina ushahidi wa kutosha dhidi ya Saif Al Islam Gaddafi - mtoto wa kiume wa kiongozi wa zamani - kumfikisha mahakamani nchini Libya.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Mkuu wa mashtaka wa ICC, Luis Moreno Ocampo - ambaye anazuru Tripoli - alisema ameambiwa kuwa Libya itatoa hoja zake kwa ICC ufikapo mwisho wa mwezi huu.

Saif Gaddafi anakabili mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu, lakini hadi sasa wakuu wa Libya wamekataa kumkabidhi kwa ICC.

Bwana Ocampo alisema ni jukumu la majaji wa ICC kutoa hukumu juu ya hoja za Libya.

Piya alisema kesi hiyo, popote pale itapofanywa, haikulekea kuanza karibuni.