Bwanaharusi Zuma avalia kijadi

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameoa mke wane, kwenye sherehe ya jadi ambapo wake zake wengine watatu piya walihudhuria.

Image caption Rais Jacob Zuma katika mavazi ya Kizulu

Bwana Zuma, mwenye umri wa miaka 70, alivaa ngozi ya chui na kubeba mkuki na ngao, mavazi ya jadi ya Kizulu, kwenye harusi iliyofanywa jimbo la KwaZulu-Natal.

Wakuu wanasisitiza kuwa Bwana Zuma mwenyewe anagharimia sherehe hizo za wikiendi hii.

Bi arusi, Bongi Ngema, amefuatana na Rais Zuma kwenye ziara zake rasmi kwa miaka kadha.