Kanisa lashambuliwa mjini Khartoum

Kanisa moja mjini Khartoum, Sudan, limechomwa moto na Waislamu.

Haki miliki ya picha AFP

Taarifa zinasema watu mia kadha waliandamana jana usiku hadi kwenye kanisa, ambalo linatumiwa na Wakristo kutoka Sudan Kusini.

Hakuna ripoti za mtu kujeruhiwa.

Sudan Kusini, ambayo watu wake wengi ni Wakristo au wafuasi wa dini za kijadi, ilipata uhuru Julai mwaka jana.

Lakini nchi mbili hizo zimeshindwa kutatua mizozo yao kuhusu visima vya mafuta na mipaka.

Mapigano yamezidi hivi karibuni katika maeneo ya mpakani, huku kuna wasiwasi kuwa vita kamili vitazuka.