Libya marufuku vyama vya kidini

Baraza la mpito la Kitaifa linasema kua sheria iliyopitishwa siku ya jumanne ilibuniwa kuhifadhi umoja wa Kitaifa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chama Moslem Brotherhood-Libya

Lakini wadadisi wanasema kua kuna uwezekano hili linaweza kuviudhi vyama vya kisiasa kama kile cha Muslim Brotherhood.

Msemaji wa Baraza la Kitaifa Mohammed al Harzy amesema kua "vyama havipaswi kuegemea dini au ukabila wala koo,"

Hata hivyo hakufafanua zaidi jinsi gani hatuia gii itaathiri chama kilichoundwa mnamo mwezi Machi cha Muslim Brotherhood pamoja na makundi mengine ya Kiislamu.

Chama hiki ndiyo chama cha nchini Libya kilichojipanga vizuri kilichotarajiwa kutoa mchango mkubwa nchini Libya ambako wafuasi wa siasa kwa misingi ya imani ya Kiislamu walididimizwa kikatili kwa kipindi cha miaka 42.

Mkuu wa kundi la Freedom and Development Party amelitaka Baraza la mpito litowe ufafanuzi zaidi na libaini maana ya kupiga marufuku vyama vyote vinavyoegemea dini.

"kipengele kama hiki ni muhimu katika nchi ambako kuna imani nyingi , na siyo Libya ambako raia wengi ni Waislamu, alisema Mohammed Sawan.

Aliongezea kusema kua sheria inafaa ichunguzwe zaidi, na ispofanyiwa marekebisho itatulazimu kufanya maandamano ya kuipinga.

Uchaguzi unaopangwa kufanyika mnamo mwezi juni utakua wa kwanza tangu mapinduzi ya mwaka jana ya Kanali Muammar Gaddafi kwa msaada wa shirika la NATO.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeshi la Libya

Kanali Gaddafi aluawa na waasi wa Libya mwezi Oktoba kufuatia miezi minane ya mapigano.