Rais Banda amtimua waziri

Rais Joyce Banda Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Joyce Banda

Kiongozi mpya wa Malawi Joyce Banda amemtimua Waziri wake wa mashauri ya kigeni, Peter Mutharika, nduguye Rais aliyefariki akiwa afisini.

Bw.Peter Mutharika alitazamiwa kama mrithi wa marehemu kakake katika uchaguzi wa mwaka 2014 wakati ikitazamiwa kua Rais aliyetoweka angestaafu.

Image caption Mazishi ya Bingu wa Mutharika

Mabadiliko haya ya baraza la mawaziri linatokea siku chache baada ya mazishi ya aliyekua Rais.

Bibi Banda alikua ni makamu wa Rais kuanzia mwaka 2009 lakini baadaye akakosana na Rais na kujitokeza kua mkosoaji wake mkali.

Bi Joyce Banda alilazimika kujiuzulu kutoka chama cha Democratic Progressive mwaka 2010 alipokaidi amri ya kumkubali Peter Mutharika awe mrithi wa rais.

Kufuatia kifo cha Bw Mutharika tareh Aprili, kulikuepo na tetesi kua washirika wa waziri wa mashauri ya kigeni wangejaribu kuzuia mkondo wa katiba wa kumkabidhi madaraka Bi Banda,ambaye tangu hapo alikua ameisha unda chama chake.