Watu 27 wajeruhiwa katika milipuko

Kituo cha Tram Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kituo cha Tram

Takriban watu 27 wamejeruhiwa kufuatia mfululizo wa milipuko katika mji wa mashariki wa Ukraine wa Dnepropetrovsk na wakuu wa huko wameuelezea kama shambulio la kigaidi.

Wizara ya dharura inasema kua milipuko minne ilitokea katika sehemu mbalimbali za mji majira ya adhuhuri.

Mlipuko wa kwanza ulitokea kwenye kituo cha Magari yajulikanayon kama tram mwendo wa saa sita kasoro dakika kumi, kwa muji=bu wa mashirika ya habari. Plipuko wa pili ukatokea karibu na jumba la sinema nusu saa baadaye. Milipuko mingine iliarifiwa kutokea katika bustan za mjini.

Taarifa za habari zimesema kua vilipuzi viliwekwa ndani ya mapipa ya taka. Watoto tisa walijeruhiwa katika mlipuko wa pili. Waziri wa masuala ya nchini wa Ukraine Vitali Zakharenko pamoja na wakuu wengine wanaelekea huko Dnep-petrovsk kuchunguza hali ya mambo.

Wakuu hao wameielezea milipuko hiyo kama kitendo cha kigaidi, ingawa bado hawajatoa sababu wala mtu au kundi kujitokeza kudai kuhusika.

Image caption Nembo ya Euro 2012 Ukraine

Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych ameielezea milipuko kama mwamko mpya na mtihani kwa nchi, ambayo katika kipindi cha chini ya miezi miwili itaandaa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya kwa ushirikiano na Poland.