Saudi Arabia yafunga ubalozi Misri

Saudi Arabia imemrudisha nyumbani balozi wake nchini Misri na imesema imefunga ofisi zake zote huko, baada ya maandamano ya hasira kulalamika juu ya wakili wa Misri wa kugombea haki za kibinaadamu kukamatwa na wakuu wa Saudi Arabia.

Haki miliki ya picha a

Ahmed El-Gizawy alikamatwa awali mwezi huu alipowasili Saudi Arabia kwa hija.

Wasaudi wanasema alijaribu kuingiza kwa magendo vitu vinavokatazwa, lakini wanaharakati wanasema el-Gizawy alikamatwa kwa sababu aliwahi kupeleka malalamiko juu ya namna wafungwa kutoka Misri wanavotendewa nchini Saudi Arabia.

Mapema juma hili, mamia ya watu waliandamana nje ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Cairo kudai wafungwa hao waachiliwe huru haraka.