Waziri wa zamani wa Libya afariki

Waziri wa mafuta wa zamani wa Libya amekutikana amekufa katika mji mkuu wa Austria, Vienna, karibu na mto Danube, kwa mujibu wa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Austria.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Shukri Ghanem, aliyekuwa na umri wa miaka 69, alikuwa mmoja kati ya wakuu maarufu waliokimbia kutoka serikali ya Kanali Gaddafi wakati wa ghasia za Libya.

Hakujatolewa maelezo zaidi, lakini inafikiriwa amekufa kutokana na ugonjwa wa moyo.

Inafikiriwa amekuwa akiishi Ulaya tangu mwezi Juni mwaka jana.