Mauaji ya kisiasa imekidhiri Burundi

Shirika moja la kutetea haki za kibinadam lililo na makoa yake mjini New York, la Human Rights Watch, limesema visa vya ghasia za kisiasa vimeongezeka sana nchini Burundi.

Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika hilo, limedai kulikuwa na mauaji ya kisiasa kila mwiki mwaka uliopita nchini humo.

Ripoti hiyo imenadi kuwa wengi wa waliouawa ni wafuasi wa upinzani na kuwa baadhi ya wanachana wa chama tawala vile vile walilengwa kwenye mauaji hayo.

Serikali ya Burundi halijasema lolote kuhusiana na matokeo ya ripoti hiyo, lakini utawala wa ncui hiyo umeizuia maafisa wa shirika hilo la Human Rights Watch kuandaa kikao na waandishi wa habari kaktika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.