Waandamanaji wajeruhi waandamanaji

Watu wasiojulikana wameua takriban waandamanaji 11 waliokua wakiandamana nje ya jengo la Wizara ya Ulinzi kupinga wakuu wa majeshi wanaotawala Misri.

Washambuliaji waliowaandama waandamanaji majira ya alfajiri walitumia mawe, virungu, mabomu na bunduki. Waandamanaji walijibu mashambulizi na kuwapiga baadhi ya washambuliaji.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamano yaendelea Misri

Askari jeshi na polisi waliweza kusimamisha mapigano hayo ingawa walifika saa sita baada ya mapigano kuanza.

Wagombea wawili wa kiti cha Rais wamesimamisha kampeni zao kama ishara ya kupinga tukio hilo.

Mgombea huru wa chama cha Independent Islamist, Abdul Moneim Aboul Fotouh, pamoja na Mohammed Mursi,huyu akiwa Kiongozi wa chama cha Freedom ana Justice tawi la Muslim Brotherhood waliwalaumu viongozi kwa kuchelewa kuchukua hatua.

Mwandishi wetu anasema kua matumizi ya majambazi yaliyovalia nguo za raia ni mbinu inayofahamika vyema kutumiwa na wakuu wa serikali.

Polisi na Majeshi waliotumwa katika eneo hilo hawakuingilia kati mapigano hayo mapema ili kusimamisha mapigano, hata alipuawa mtu mmoja katika mapigano kama haya mnamo siku ya jumapili.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Muandamanaji ashuhudia mlipuko

Wizara ya Afya imesema kua zaidi ya watu 150 wamejeruhiwa na kwammba wengi wanapokea matibabu kwenye zahanati iliyo karibu na eneo la tukio. Baadhi wana majeraha ya risasi huku wengine wakiwa na majeraha ya visu.

Mshindi wa tuzo ya Nobel aliyekua Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalochunguza suala la Nuclear, Mohamed El Baradei amewalaumu wakuu wa serikali kupitia mtandao wa Twitter.

Wakuu hao wa Kijeshi waliahidi kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia kabla ya mwisho wamwezi juni, baada ya Uchaguzi wa Rais.