Kikwete asuka baraza

Jakaya
Image caption Rais wa Tanzania amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amewafuta kazi mawaziri waandamizi katika baraza lake la mawaziri. Katika mabadiliko hayo, waziri wa fedha Mustapha Mkullo ni miongoni mwa waliowekwa kando.

Mawaziri wapya waliochukua nafasi mpya kuwapisha walioachwa ni kama ifuatavyo (walioachwa majina kwenye mabano), Waziri wa Nishati na Madini - Profesa Sospeter Muhongo (William Ngeleja), Waziri wa Fedha - Dr William Mgimwa ( Mustapha Mkullo), Waziri wa Uchukuzi - Dr Harrison Mwakyembe (Omar Nundu), Waziri wa Maliasili na Utalii - Khamis Kagasheki (Ezekiel Maige), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii - Dr Hussein Mwinyi (Dr Haji Mponda) na Waziri wa Viwanda na Biashara - Dr Abdallah Kigoda (Dr Cyril Chami).

Ubadhirifu

Kabla ya kusoma orodha hiyo mpya, Rais Kikwete alisema majadiliano ya kina yamefanyika na wenzake kabla ya kuikamilisha, "Tumeona wawili kati ya wale tunaweza kuwahamishia katika wizara nyingine, lakini tukitazama baraza zima kwa ujumla wake, tumewapanga hapa na pale kuwabadilisha baadhi ya wizara ili kuimarisha utendaji. Hatujabadili idadi ya wizara, tulikuwa na mjadala mkali kidogo na wa kina kidogo - ipo rai kuwa wizara hiyo imekuwa kubwa mno".

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambaye alibainisha hitilafu kadhaa za ubadhirifu wa fedha za umma kwenye wizara hizo.

Fedha za umma

Sura nyingi mpya zipo katika nafasi za manaibu waziri. Miongoni mwao ni January Makamba anayechukua unaibu waziri kwenye Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia, akina mama wawili Saada Mkuya Salum akiwa naibu waziri wa fedha kutokea Zanzibar bega kwa bega na mwenzake mpya Janet Mbene anayesimamia wadhifa huo huo kwa upande wa Tanzania bara.

Vile vile Rais Kikwete kwa mara ya kwanza amewateua manaibu waziri wawili kusaidiana majukumu kwenye Wizara ya Nishati na Madini.

Mabadiliko hayo yamekuwa yakisubiriwa kwa muda tangu mjadala mkali ulipozuka bungeni kuwahusu mawaziri ambao wizara zao zilituhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa kiasi kikubwa cha fedha za umma.

Hata hivyo Rais Kikwete amewaeleza watanzania kuwa kuanzia sasa, uwajibika wa aina hiyo utawahusu maaafisa waandamizi wote katika wizara husika.

ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora) Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI) Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO) Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3. OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza, Mb.,

Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

5. NAIBU MAWAZIRI

OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI

6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

7. OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8. WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,

Wataapishwa Jumatatu tarehe 8 Mei, 2012 saa 5.00 asubuhi katika viwanja vya Ikulu