Gereza yashambuliwa Nigeria

Watu waliokuwa na silaha wamevamia gereza nchini Nigeria katika jimbo la Borno, kaskazini-mashariki mwa nchi, na kuwauwa walinzi wawili, na kuwaachilia huru wafungwa.

Haki miliki ya picha Reuters

Polisi walisema wapiganaji wa kikundi cha Waislamu cha Boko Haram walishambulia kituo cha polisi kwenye mji wa Banki, kabla ya kuelekea gerezani karibu na kijiji cha Kunshi.

Msemaji wa polisi alieleza kuwa wamewakamata watu 23.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo, lakini Boko Haram imelaumiwa kwa matukio kadha ya mauaji nchini Nigeria.