Kiongozi wa zamani wa Kuwait asailiwa

Imebadilishwa: 6 Mei, 2012 - Saa 13:52 GMT

Taarifa za vyombo vya habari vya Kuwait zinaeleza kuwa jopo la mahakama limemhoji waziri mkuu wa zamani, Sheikh Nasser al-Mohammad al-Sabah, kuhusu tuhuma kuwa alighushi dola mamia ya mamilioni na kuziweka kwenye akiba zake za benki nchi za ng'ambo.

Maandamano nje ya bunge la Kuwait, kutaka waziri mkuu wa zamani ajiuzulu.

Sheikh Nasser, ambaye alijiuzulu mwezi wa Novemba, anakanusha tuhuma hizo.

Vyombo vya habari vya Kuwait, vinaeleza kuwa aliyerithi nafasi ya Sheik Nasser, Sheikh Jaber Mubarak al-Sabah, amezungumza mbele ya jopo la bunge linalochunguza kisa hicho piya.

Viongozi wote hao wawili ni wa ukoo ulioongoza Kuwait kwa zaidi ya karne mbili na nusu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.