Niger ni hatari kwa akina mama

Imebadilishwa: 8 Mei, 2012 - Saa 11:28 GMT

Mama na watoto Niger


Nchi ya Magharibi mwa Afrika ya Niger ndiyo mahala pabaya zaidi duniani kwa akina mama kuishi kulingana na ripoti ya shirika la kuwahudumia watoto la Save the Children.

Hili limejitokeza katika orodha ya shirika hilo ya kila mwaka inayolinganisha mazingira wanamoishi akina mama katika nchi 165.

Ripoti hiyo inazingatia mambo mbali mbali ikiwemo afya , elimu , uchumi na lishe bora. Kwa sasa Niger inakumbwa na uhaba wa chakula. Nchi hiyo inachukua nafasi ya Afghanistan iliyokuwa inashikilia nafasi ya mwisho kwenye orodha hiyo kwa miaka miwili iliyopita.

Mwaka huu hali nchini Niger inaonyesha sana athari za ukosefu wa lishe bora kwa wamama.

Tatizo la chakula ambalo limekithiri katika eneo la Sahel linatishia maisha ya mamilioni ya watoto , kulingana na shirika la Save the Children.

Shirika hilo limeelezea ambavyo ukosefu wa chakula unawafanya akina mama ambao wenyewe waliathirika kutokana na ukosefu wa lishe bora,kujifungua watoto wenye uzani wa chini.

Ripoti hiyo inaonya kuwa ikiwa mama anakosa lishe bora , na anafanyishwa kazi nyingi , akiwa hana kisomo pamoja na kuwa na afya ambaya hawezi kumpa lishe bora mtoto wake, athari zake zikiwa mbaya sana.

Mkuu wa sera katika shirika hilo, Brendan Cox amesema kuwa kuna haja ya uongozi mzuri duniani kuhusu swala la utapia mlo, ambao utachangia kuwepo miradi nzuri ya afya kwa niaba ya akina mama na watoto wao ili kuhakikisha afya nzuri na uhai katika eneo hilo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.