Uchina yakanusha kuwa yaandaa vita

Uchina imekanusha ripoti kuwa jeshi lake linajitayarisha kwa vita, katika mvutano kuhusu eneo lenye mzozo la bahari ya Kusini ya Uchina.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Shirika la habari la taifa limeionya Ufilipino, kwamba vita vinaweza kutokea juu ya mashindano ya hivi sasa kwa sababu ya mzozo kuhusu mwamba ulioko nje ya mwambao wa Ufilipino.

Lakini wizara ya ulinzi ya Uchina imekanusha tuhuma hizo kuwa iko tayari, na kwamba eneo la Guangzhou la kusini mwa Uchina linajiandaa kwa vita.

Meli za Uchina na Ufilipino zimekuwa zikizozana kwa zaidi ya mwezi mmoja kwenye majabali yanayoitwa Scarborough Shoal.