Gaidi asakwa Kenya

Imebadilishwa: 12 Mei, 2012 - Saa 14:46 GMT

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamesema wanamsaka raia mmoja kutoka Ujerumani anayetuhumiwa kuhusika na mashambulio ya hivi karibuni nchini humo.

Raia wa Uingereza aliyefikishwa mahakamani Mombasa kwa tuhuma za ugaidi

Mtu huyo kwa jina Ahmed Khaled Mueller anadaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la al- Shabaab.

Kenya imeshambuliwa mara kadhaa tangu majeshi yake kuingia nchini Somalia kuwasaka wapiganaji wa Al shabaab.

Mmwandishi wa BBC mjini Nairobi anaarifu kuwa maafisa wa polisi nchini Kenya wametoa picha ya raia huyo kwa jina la Ahmed Khaled Mueller na kusema ana uhusiano wa karibu na kundi la al- Shabaab.

Japo maafisa wa polisi hawasemi ni lini aliingia nchini Kenya, wanasema aliingia nchini kinyume cha sheria na kwamba amejihami.

Aidha, polisi imesema mtu huyo anadaiwa kuhusika na mashabulizi ya hivi karibuni nchini.

Hii sio mara ya kwanza kwa polisi kutoa picha ya mtu anayeshukiwa kuhusika na kupanga mashambulizi nchini Kenya.

Mapema mwaka huu, polisi ilitoa picha ya raia mmoja wa Uingereza ambaye anadaiwa kuhusika na kupanga mashambulizi pwani mwa Kenya, na wiki iliyopita maafisa wa polisi walichapisha picha nyengine ya mtu anayedaiwa kuhusika na shambulio la guruneti la mwezi wa Aprili, katika kanisa moja mjini Nairobi, mbapo watu wawili waliuwawa na zaidi ya 15 kujeruhiwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.