Wasudan Kusini kurudishwa toka Khartoum

Imebadilishwa: 14 Mei, 2012 - Saa 03:43 GMT

Kundi la kwanza la wakimbizi wa Sudan Kusini ambao walikuwa wamekwama katika kambi za Sudan waanza kuelekea nyumbani.

Mtoto katika kambi ya wakimbizi wa Sudan Kusini iliyo Sudan

Karibu raia 400 wa Sudan kusini waanza kusafirishwa kwa mabasi toka Khartoum ambapo baadaye watasafirishwa kwa ndege hadi Juba,mji mkuu wa Sudan.

Kuna zaidi ya wasudan Kusini 15,000 ambao wamekwama Sudan baada ya kupewa makataa ya kuhama Khartoum.

Mwezi uliopita wakimbizi hao walitajwa kama tishio kwa usalama wa Sudan na waliamriwa waondoke na warudi kwao Sudan Kusini.

Agizo hilo la kuhama ni baada ya Sudan Kusini kupata uhuru hivyo basi raia wake waliokuwa wakiishi Sudan kuambiwa kuwa wamepoteza uraia wao.

Shughuli hiyo yakuanza kuwasafirisha raia hao wa Sudan Kusini kunafuatia hatua ya Mkuu wa shirika la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa Navi Pillay kuishutumu Sudan kwa kuishambulia Sudan Kusini kwa mabomu licha ya kuagizwa na umoja wamatifa kumaliza uhasama kati yao.

Siku ya jumatano Sudan kusini iliilaumu jirani yake Sudan kwa kushambulia maeneo yake kwa mabomu lakini Sudan ikajibu kwa kusema kuwa inahaki yakujibu mashambulizi yeyote.

Mipango ya kuwasafirisha wasudan kusini kutoka maeneo kama vile Kosti yalio white Nile yanafanywa na shirika la kusaidia wakimbizi la IOM.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.