Benghazi yachagua serikali ya mji

Wananchi wa Libya wanapiga kura kuchagua baraza la mji wa Bengazi, mji uliokuwa kitovu cha mapinduzi yaliyomtoa madarakani Kanali Gaddafi.

Haki miliki ya picha Reuters

Hii ni mara ya kwanza kwa wakaazi wa Benghazi kupiga kura kwa muda wa karibu miaka 50, na imetengazwa ni kuwa siku ya mapumziko.

Watu kama laki-mbili wamejiandikisha kupiga kura, na watu zaidi ya 400 wanagombea viti 41 vya baraza la jiji.

Mwezi ujao, Libya itafanya uchaguzi wa bunge.