Chen asema yuko njiani kuondoka Beijing

Mwanaharakati kipofu wa Uchina anayetetea sheria, ambaye amekuwa chanzo cha mzozo wa kidiplomasia kati ya Uchina na Marekani, amesema yuko uwanja wa ndege wa Beijing, akitarajia kwenda Marekani.

Haki miliki ya picha AP

Hapo awali Chen Guangcheng alitoka hospitali ambako alikuwa amezuwiliwa tangu aondoke katika hifadhi ya ubalozi wa Marekani.

Bwana Chen alisema yeye pamoja na mkewe na watoto wawili hawakuwa na paspoti, lakini wakitaraji kupewa na maafisa wa Uchina.

Mara nyingi amesema kuwa ana wasi-wasi juu jamaa zake wengine, ambao wanasema kuwa walibughudhiwa baada ya Bwana Chen kutoroka kifungo cha nyumbani mwezi uliopita.