Mashambulio mawili yafanywa Mogadishu

Watu kadha wameuwawa katika mashambulio mawili mjini Mogadishu, Somalia.

Haki miliki ya picha AP

Bomu moja liliripuka kando ya barabara, katika mtaa wa Karan, kaskazini mwa jiji, ambalo inaarifiwa liliuwa kama wanajeshi wane wa serikali.

Na kwenye tukio jengine maguruneti mawili yalirushiwa polisi, walipokuwa wakifyeka makaazi kwenye soko ya Bakara.

Mchuuzi kwenye soko hilo ameiambia BBC, kwamba mtu mmoja aliuwawa na wengine wane walijeruhiwa.

Mji wa Mogadishu unadhibitiwa na wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Afrika; lakini wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab wameendelea kufanya mashambulio mjini humo.