Wategua mabomu waachiliwa huru Sudan

Imebadilishwa: 20 Mei, 2012 - Saa 15:04 GMT


Sudan imewaachilia huru wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaotegua mabomu, ambao walikamatwa mwezi uliopita karibu na mpaka wa Sudan Kusini.

Thabo Mbeki, mpatanishi wa AU, Sudan

Katika sherehe iliyofanywa mjini Khartoum, maafisa hao walikabidhiwa kwa rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, ambaye anapatanisha baina ya Sudan na Sudan Kusini kwa niaba ya Umoja wa Afrika, AU.

Watu hao wane, kutoka Uingereza, Norway, Afrika Kusini, na Sudan Kusini, walikamatwa wakikusanya mabaki ya vita, katika eneo la mafuta la Heglig, lenye mzozo.

Wakijaribu kuchunguza aina ya silaha zinazotumiwa na pande zote mbili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.