Afisa wa haki za binaadamu afika Harare

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulika na haki za kibinaadamu, anazuru Zimbabwe kwa mara ya kwanza.

Haki miliki ya picha Reuters

Bi Navi Pillay amealikwa na serikali ya Zimbabwe kwa ziara ya siku tano - hatua ambayo mwandishi wa BBC anasema, isingetokea miaka michache iliyopita.

Serikali ya Zimbabwe hivi karibuni imekuwa na hamu ya kuimarisha sura yake, wakati inajaribu kuomba vikwazo vya kimataifa dhidi ya nchi hiyo viondoshwe.

Vikwazo viliwekwa kwa sababu nchi hiyo ikikiuka haki za kibinaadamu.

Bi Pillay anatarajiwa kukutana na Rais Robert Mugabe, lakini piya anapanga kuzungumza na makundi ya kutetea haki za kibinaadamu nchini Zimbabwe.