Msanii wa Begees Robin afariki

Haki miliki ya picha ap
Image caption Bendi ya Bee Gees, Robin Gibb ( kushoto)

Tangazo hili lilitolea na familia yake kwa huzuni mkubwa. Gibbs ambaye ni mzaliwa wa Uingereza, alianza sanaa ya muziki alipounda bendi ya Bee Gees na kaka zake, Barry na Maurice mwaka 1958.

Bendi hiyo ilikuwa mojawapo ya bendi zilizokuwa maarufu sana na zenye kuuza rekodi nyingi sana kwa zaidi ya miaka hamsini ikiwemo nyimbo kama Stayin' Alive, How Deep Is Your Love, Massachusetts na Night Fever.

Familia ya Gibb ilitangaza kuwa msanii huyo aliyekuwa na miaka 62 alifariki kutokana na saranati aliyougua kwa muda mrefu pamoja na upasuaji wa tumbo.

Mwandishi habari mmoja, Paul Gambaccini amemtaja mwanamuziki huyo kama mojawapo ya wasanii wakubwa katika historia ya Uingereza.

Nduguzake Gibb, walizaliwa katika kisiwa cha Isle of Man ingawa walikulia Manchester, na baadaye kuhamia nchini Australia.

Bee Gees walitoa album ambazo ziliwaletea mauzo ya mamilioni ya dola kote duniani tangu kuanza kwa bendi hiyo miaka ya tisini.

Gambaccini alisema bendi hiyo ya Bee Gees inaweza tu kufanananishwa na wanamuziki kama Lennon na McCartney kama wanamuziki waliofanikiwa sana katika sanaa ya muziki nchini Uingereza.